Ukiishi Mexico City katika daraja la watu wakubwa na wewe na anasa ni marafiki wakubwa, hutapenda kuendesha gari ambayo kila mtu anaendesha mjini. Nunua gari na kuibadilisha kuwa ya kwako. Lisa aliponunua gari yake huko Ejército Nacional Mexicano, Mexico City, katika duka la Ferrari, aliipeleka Los Angeles kwa marekebisho aliyoyataka. Ferrari haikuwa ya kawaida. Mbali na kinga ya risasi ya inchi nne, Ferrari ya Lisa ilikuwa na mwendo mkali na matairi makubwa kuliko Ferrari za kawaida. Ilikuwa na rangi tatu: nyeusi, pinki na njano zilizokuwa zikibadilika kulingana na hali ya hewa; na kadhalika ilikuwa na breki ya upepo kwa nyuma, katika buti ya aluminiamu, kwa ajili ya kuikandamiza chini wakati wa mwendo mkali, ili isiyumbe sana barabarani. Lisa peke yake ndiye aliyekuwa na gari ya namna hiyo Mexico City nzima.

Enock Maregesi

Tags: snooty exclusivity



Go to quote


Gari hii ni nzuri kuendesha.

Enock Maregesi

Tags: snooty exclusivity



Go to quote


Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine.

Enock Maregesi

Tags: truth untruth



Go to quote


Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona. Ndoto yako waijua mwenyewe.

Enock Maregesi

Tags: inspirational



Go to quote


Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.

Enock Maregesi

Tags: informational



Go to quote


Joram Kiango ni mpelelezi maarufu nchini Tanzania. Willy Gamba ni mpelelezi maarufu katika bara la Afrika. John Murphy ni mpelelezi maarufu duniani. Ni watu watatu tofauti wanaofanya kazi zinazofanana.

Enock Maregesi

Tags: informational



Go to quote


Kinachotokea leo kitatuathiri kesho. Mbegu tunazopanda sasa ni mazao ya msimu ujao.

Enock Maregesi

Tags: inspirational



Go to quote


Kufanya kosa huku ukijua ni kosa ni kujiombea jela mwenyewe.

Enock Maregesi

Tags: inspirational



Go to quote


Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.

Enock Maregesi

Tags: drug-addiction



Go to quote


Watu wanapokuwa katika migogoro maisha yao hutakiwa kurahisishwa. Kuna ukingo mwembamba kati ya uzima na wazimu.

Enock Maregesi

Tags: inspirational-attitude



Go to quote



Page 1 of 10.
next last »

©gutesprueche.com

Data privacy

Imprint
Contact
Wir benutzen Cookies

Diese Website verwendet Cookies, um Ihnen die bestmögliche Funktionalität bieten zu können.

OK Ich lehne Cookies ab